HAJI MANARA AITAKA TCRA IMCHUKULIE HATUA SHABIKI WA YANGA ALIYEWAZUSHIA AJALI WACHEZAJI WA SIMBA NA KOCHA WAO

MSEMAJI wa Simba, Haji Manara ameomba kuchukuliwa hatua kwa shabiki wa Yanga, Pascal Lameck aliyeposti kwenye mtandao wa kijamii wa facebook taarifa ya uongo kuwa basi la wachezaji wa Simba limepata ajali na wachezaji wote wamevunjika mguu, huku kocha wao, Joseph Omog akiwa hajulikani alipo.

Kupitia posti aliyoitoa kwenye mtandao wa facebook, Manara alihoji uhalali wa shabiki huyo kuendelea kuwepo uraiani akitazamwa tu bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka ya mawasiliano ya TCRA.

“Always huwa najiuliza mashabiki wa aina hii tunawaacha kwa nini? Na TCRA ichukue hatua, tusingoje hadi watukanwe wakubwa tu, hatuwezi kusamehe kila kitu,” ameandika Manara kwenye posti yake aliyoiambatanisha na posti ya shabiki huyo. 

No comments