HANS PLUIJIM AMPIGIA SALUTI GEORGE LWANDAMINA KWA KUIONGOZA YANGA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU

KOCHA wa Singida United, Hans Van der Plujim amepongeza jitihada zilizofanywa na George Lwandamina ambaye ameisaidia Yanga kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika msimu wake wa kwanza.

Plujim alisema Yanga walistahili ubingwa kutokana na ubora wa kikosi chake pamoja na jitihada zilizofanywa na Lwandamina kuiweka timu pamoja.

“Unaweza kuona ni kwa namna gani kocha alikuwa na kazi kubwa kuitengeneza timu ya ushindi huku kukiwa na matatizo lukuki yanayohusu fedha, halikuwa jambo rahisi kufika mafanikio aliyopata,” alisema Plujim.

“Walistahili kupata walichopata, wamepambana pamoja tangu mwanzo wa msimu mpaka hatua ya mwisho, nadhani Lwandamina atakuwa ni mwenye furaha wakati huu,” aliongeza.


Kabla ya kutua Singida United, Plujim aliiongoza Yanga kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara mbili mfululizo sambamba na Kombe la FA ambalo linafanikiwa kubeba msimu uliopita.

No comments