HANS PLUIJIM ANASA NYOTA WA ZAMANI WA MAMELODI SUNDOWNS

KOCHA wa timu ya Singida United, Hans Pluijim amekuwa akifanya jambo jipya kwenye kikosi chake kila baada ya wiki.

Kocha huyo aliyewahi kuinoa Yanga kwa mafanikio makubwa amefanikiwa kunasa mchezaji mwingine aliyekuwa anaitumikia timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Nhivi Simbarashe ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Caps United ya nchini Zimbabwe.

Timu hiyo iliyopanda daraja imekamilisha usajili wa nyota huyo baada ya kumpa mkataba wa miaka miwili.

“Tumekamilisha taratibu zote za usajili na tayari tumempa mkataba wa miaka miwili, ni mchezaji mzoefu ambaye atatusaidia kwenye michuano ya Ligi Kuubara,” alisema mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Festo Sanga.


Mpaka sasa klabu hiyo imefanikiwa kunasa wachezaji watano wa kigeni wakiwemo Twafaza Kutinyu, Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa na Mganda Shafik Batambuze ambaye walimtambulisha wiki moja nyuma.

No comments