HANSCANA AJIVUNIA KIFIKIA MALENGO ALIYOJIWEKEA KIMUZIKI MWAKA HUU

MUONGOZAJI anayetamba kwa kutoa video kali kwa sasa Bongo, Hanscana amejikuta akifikia malengo aliyojiwekea kwa mwaka huu ya kutoa video 12 ikiwa imesalia miezi sita na siku kadhaa kabla ya mwaka 2017 kumalizika.

Kupitia mtandao wake wakijamii wa Instagram Hanscana aliandika: “Mwaka 2017 nilipanga kushoot Video 12 tu."

“Nilitangaza hivyo mwanzoni mwa mwezi Januari ila mpaka inafika Februali nilikuwa nimefanya mara tatu za idadi na mpaka sasa nishatoa video 11 na kufanya video 26 ni jambo la kumshukuru Mungu."


Alisema wiki hii atatoa video ya 12 kutoka kwa msanii ambae tangu waanze kufanya kazi pamoja hajawahi kushoot kwingine hata kwa bahati mbaya.

No comments