HASSAN KESSY ACHEKELEA TIMU YAKE YA YANGA KUBEBA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

BEKI wa Yanga aliyekuwa na majanga kabla ya msimu kumalizika, Hassan Kessy ameonyesha furaha baada ya kukata kiu yake ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu bara  akiwa sehemu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza.

Kessy alitua Yanga mwishoni mwa msimu uliopita baada ya  vuta nikuvute  ya muda mrefu huku  klabu yake ya Simba ikidai kuwa na mkataba nae  kabla ya nyota huyo kuidhinishwa kuchezea Yanga.

‘’Nimebahatika kuchezea timu zote kubwa hapa nchini  kasoro Azam lakini kubwa zaidi ni kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara nikiwa ndani ya kikosi cha kwanza," alisema Kessy. 

"Hakuna asiyejua misukosuko niliyokumbana nayo na namna ambavyo  nililazimika kukaa nje ya kikosi ili kupisha  mvutano uliokuwepo lakini sasa kila kitu kimebadilika, aliongeza nyota huyo.


Beki huyo ataungana na baadhi ya nyota wageni  kusherehekea ubingwa wakimemo Justine Zulu, Beno Kakolanya, Andrew Vicent na Emanuel Martin.

No comments