HATIMAYE ARSENAL YAAMBULIA TAJI LA FA, CHELSEA HOI


Arsenal imefanikiwa kuokoa msimu wao kwa kubeba taji la FA baada ya kuinyuka Chelsea 2-1 katika mchezo mkali wa fainali.

Kikosi cha Wenger kilikuwa hatarini kumaliza msimu bila taji, lakini magoli ya Sanchez dakika ya 4 na Ramsey dakika ya 79, yalitosha kuwazima Chelsea waliokuwa wamepania kutwaa mataji mawili.

Bao pekee la Chelsea lilifungwa na Diego Costa kunako dakika ya 76.

ARSENAL: Ospina, Holding, Mertesacker, Monreal, Bellerin, Ramsey, Xhaka, Oxlade-Chamberlain (Coquelin 82), Sanchez (Elneny 90+3), Ozil, Welbeck (Giroud 78).

CHELSEA: Courtois, Azpilicueta, Luiz, Cahill, Moses, Kante, Matic (Fabregas 61), Alonso, Pedro (Willian 72), Costa (Batshuayi 88), Hazard.
Sanchez anaanza kutimua mbio kushangilia goli lake
Diego Costa baada ya kuisawazishia Chelsea
Ramsey (kulia) akishangilia bao la ushindi No comments