HATMA YA WENGER MASHAKANI … ATOA SHARTI GUMU ARSENAL


Arsene Wenger amejiweka mwenyewe kwenye kona ngumu juu ya hatma yake Arsenal.

Wenger amewaambiwa waandishi wa habari kuwa atakataa kufanya kazi na mkurugenzi wa soka na anataka madaraka kamili juu ya benchi la ufundi.

Hivi karibuni Arsenal ilitoa taarifa kuwa klabu hiyo itaajiri mkurugenzi wa soka ambaye atakuwa na sauti ya mwisho juu ya usajili na mikataba ya wachezaji, nafasi ambayo haikuwahi kuwepo Emirates hapo kabla.

Lakini Wenger ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu, akasema: “Sielewi kabisa mkurugenzi wa ufundi ana kazi gani.

“Je ni mtu anayesimama barababarini na kuelekeza cheza kushoto na kulia? Sielewi kabisa na siwezi kuelewa majukumu yake.

“Mimi ni meneja wa klabu ya Arsenal na kadri nItakavyoendelea kuwa meneja, nitakuwa na kauli ya mwisho juu ya mambo yote ya soka ikiwemo benchi la ufundi.


“Baadhi ya makocha wanapendelea kuwa na jukumu moja tu - la kufundisha timu – na wanafurahia hilo. Mimi si aina ya watu hao”.

No comments