HAWA KASOMO AANZA AANZA MAZOEZI MEPESI KUJIANDAA KUREJEA JUKWAANI

MWIMBAJI aliyeanzia kwenye unenguaji, Hawa Kasomo amesema kuwa ameanza kuchukua mazoezi madogomadogo kwa ajili ya kujiweka sawa kabla hajarejea tena jukwaani kukata kiu ya mashabiki wanaomwitaji arudi kuwaburudisha.

Akiongea na saluti5, Hawa aliyejitumbukiza kwenye unenguaji kwa kuvutwa na Taabu Mambosasa, amesema kuwa aliamua kupumzika shughuli za muziki na kugeukia ujasiriamali kwa muda, lakini hivi sasa anajipanga kuibuka upya.

“Nimeanza kufanya mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiweka sawa kabla sijarudi tena jukwaani, najua mashabiki wangu wamenimiss sana ila nawaambia wasijali kwani muda si mrefu wataanza kuniona tena,” amesema.

Hawa amesema kuwa hivi sasa kuna mazungumzo yanaendelea kati yake na viongozi wa kundi ambalo naye ni mmoja wa waasisi, Kalunde Band, ambapo kama mipango itakwenda sawa atarejea tena kwenye bendi hiyo iliyo chini ya Deo Mwanambilimbi.  

No comments