HIMID MAO AFUZU KUCHEZA SOKA LA KULIPWA DENMARK

MTANZANIA Himid Mao Mkami amefuzu kucheza soka la kulipwa nchini Denmark katika klabu ya Randers FC ambayo inashiriki Ligi Kuu.

Himid Mao alikwenda kufanya majaribio ya siku 10 katika timu hiyo inayonolewa na kocha Olafur Kristjsnsson.

Himid Mao maarufu kwa jina la "Ninja" anatoka kwenye familia ya mpira baada ya baba yake Mao Mkami kuichezea Pamba kwa mafanikio makubwa.

Mao anakuwa Mtanzania wa tatu kucheza soka Ulaya kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu kwenye ukanda wa nchi za Ulaya Mashariki.

Mao Mkami amechezea Azam tangu akiwa na timu ya vijana na msimu huu amefanikiwa kuipa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.


Nyota wengine ambao wapo ukanda huo ni pamoja na Mbwana Samatta aliye chini ya Ubelgij na Thomas Ulimwengu ambaye yupo Sweden.

No comments