KIUNGO wa timu ya Azam FC, Himid Mao Mkwami anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi cha Randers ambacho kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AC Horsens ikiwa kama sehemu ya majaribio yake.

Taarifa kutoka kwenye timu hiyo zinasema kuwa Himid amekamilika kwa kila kitu na ana uwezo wa kucheza kwenye Ligi Kuu ya Denmark ikiwa tu atafuzu kwenye hatua ya majaribio.

Kiungo huyo aliondoka nchini na kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Randers ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Denmark na atakuwa huko kwa muda wa simu kumi.

Himid atapewa nafasi kwenye mechi za majaribio ambazo hujumuisha nyota wa kikosi cha pili, ili aweze kuonyesha uwezo wake.

Hata hivyo, taarifa zilizopo ni kuwa nyota huyo ana nafasi kubwa ya kufuzu majaribio baada ya kuanza kulivutia benchi la ufundi katika mazoezi ya awali aliyofanya na kikosi cha kwanza.


Himid atakuwa nyota wa tatu kucheza Ulaya katika timu zinazoshiriki Ligi Kuu baada ya Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambaye yuko Sweden.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

Oldest posts

 
Top
Nicolaus Trac