HISTORIA MPYA: JOKHA KASSIM KUPANDA JUKWAA LA JAHAZI KWA MARA YA KWANZA MEI 13


Mwimbaji nyota wa taarab, Jokha Kassim, ataandika historia mpya kwa kupanda jukwaa la Jahazi Modern Taarab kwa mara ya kwanza tangu kundi hilo lianzishwe miaka 11 iliyopita.

Jokha Kassim atashiriki onyesho la Jahazi Mei 13 ndani ya ukumbi wa Dar Live, Mbagala.

Mwimbaji huyo ambaye ameimba nyimbo kadhaa zilizohusishwa na madongo kwenda Jahazi, hatakuwa peke yake bali pia atakuwa na mkongwe Sabah Muchacho.

Kihistoria hata Sabah naye hakuwahi kupanda jukwaa la Jahazi hapo kabla na hivyo kulifanya onyesho hilo liwe na msisimko wa aina yake.

Mratibu wa onyesho hilo Juma Mbizo ameiambia Saluti5 kuwa show hiyo imepewa jina la “Usiku wa Ustaarabu wa Pwani.

Mfalme wa Kibao Kata Kivurande Junior naye atakuwa sehemu ya wasanii watakaotumbuiza katika onyesho hilo kubwa.

No comments