HUSSEIN MACHOZI AFICHUA SABABU YA KUINGIA LEBO YA MAN WATER

MSANII wa bongofleva, Hussein Machozi mara nyingi hufanya kazi zake mwenyewe lakini kwa sasa ameamua kuwa chini ya lebo ya Man Water katika kibao chake kinachokwenda kwa jina la ‘Nipe Sikuachi’, katika studio ya Combination Sound.

Akiongea na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam jana, Hussein Machozi alielezea sababu zilizomfanya awe chini ya usimamizi wa Man Water akisema: “Man Water kwanza anajua kufanya kazi na kila kazi yake huwa inabamba sana, hajawahi kukosea, pili ni mshikaji wangu toka kitambo.”

Msanii huyo  ameahidi kurudi kwa kishindo baada ya kupotea kwa muda mrefu kwenye muziki aligusia kuwa yeye kama mwanamuziki hapendi kujaribu hivyo atasimama kwa miguu yote miwili,na amewahakikishia mashabiki wake kufanya kazi nzuri zadi.


Hussein Machozi ambae anatambulika kwa nyimbo zake kali ikiwemo ‘Utaipenda’ na nyinginezo ambazo zilichangia kumuweka juu na kumfanya awe na jina kubwa kwenye muziki.

No comments