HUSSEIN MACHOZI AFICHUA SIRI NZITO YA MAISHA YAKE... asema hajawahi kumuona baba yake mzazi

PENGINE inaweza kuwa ni siri ambayo wengi hawakuwahi kuifahamu hapo kabla lakini sasa mwenyewe, msanii wa bongofleva Hussein Machozi ameamua kuianika bayana kuwa hamjui baba yake mzazi.

Machozi ambaye jana aliachia rasmi chupa lake la “Nipe Sikuachi” amesema mama yake aliwahi kumsimulia tu kwamba baba yake alipotelea machimboni kwa kufukiwa na kifusi alipokuwa katika mihangaiko ya kuitafutia maisha familia yake.

“Nimeishi maisha ya kutangatanga sana na mama yangu tukiangaika na mizigo kichwani kila uchao mara huku mara kule kutokana na hali hiyo, ambapo wakati mwingine tuliteseka na njaa kutokana na kukosa chakula,” amefichua Machozi kwa masikitiko.


“Hadi natoa singo yangu ya “Kwa Ajili Yako” bado maisha yangu yalikuwa hayaeleweki kabisa na kama mtu ningemuoinyesha ghetto nililokuwa naishi wakati huo angechoka,” amesema msanii huyo ambaye hivi sasa yuko chini ya lebo ya Combination Sound.

No comments