HUSSEIN MACHOZI AMCHAGUA HARMORAPA NA KUMUACHA JUMA JUX... asema anamuhesabu kama ni Diamond Platnumz wa pili

UKIMWULIZA Huissein Machozi msanii gani anayemkubali na ambaye yuko tayari kupiga nae kolabo, kati ya Juma Jux na Harmorapa, atakwambia Hamorapa ambaye binafsi anamchukulia kama Diamond Platnumz mpya.

Machozi anasema moja ya vitu vinavyomfanya amkubali Harmorapa ni namna anavyoweza kucheza na “show bize” ambayo hata yeye anatamani kuifanya ila anashindwa kutokana na uwezo mdogo alionao.

“Harmorapa ni msanii ambaye akinambia hata kwa kunilazimisha kwamba anataka kufanya vocal kwenye ngoma yangu, namruhusu kwasababu najua zile show bize anazozifanya zitanisaidia kwasababu mimi sina,” amesema Machozi.


“Harmorapa ni underground kwa sasa, hebu nambie baada ya miaka miwili au mitatu mbele atakuwaje?” amesema Machozi ambaye anaishi nchini Italia lakini kwa sasa yuko nyumbani Bongo kwa mapumziko ya mwezi mmoja na nusu.

No comments