HUSSEIN MACHOZI ASIFU VIDEO YA "NIPE SIKUACHI" ALIYOIFANYIA ITALIA... aponda wasanii kukimbilia "kushutia" Afrika Kusini

HUSSEIN Machozi amelimiminia sifa chupa la wimbo wake mpya wa “Nipe Sikuachi” lililoachiwa rasmi leo na kusema kuwa ni moto wa kuoteambali na linakuja kuonyesha picha ya mabadiliko katika sekta hiyo.

“Video yangu mimi nimefanyia Italia na naamini ni bonge la amazing kwasababu Wabongo wengi hawajazoea kuona video za bongofleva ina barafu na hii yangu inaweza kuwa ya kwanza,” amesema.

Amesema hakufikiria kwenda kufanya video hiyo Afrika Kusini akidai kuwa haoni tofauti ya mtu aliyechukua picha za video Afrika Kusini na yule aliyefanyia hapa nyumbani kwani mazingira ya nchi hizo yanafanana kwa kiasi kikubwa.

“Kuna vitu fulani vinakuwepo tu, yaani kama ni maghorofa tunayo mengi mjini, swimming pool za kumwaga so huwezi kunidanganya… angalia goma hili ndani kuna barafu, Tanzania hakuna wala huko South Afrika wanakokimbilia wasanii wengine wengi,” amesema.

No comments