HUSSEIN MACHOZI ATANGAZA KUMSAMEHE MENEJA WAKE "ALIYEMTOKEA" MKEWE

STAA wa bongofleva, Hussein Machozi amesema amemsamehe mdau wake mkubwa wa muziki aliyekuwa akimsimamia mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambaye aliteleza na kumtamkia neno la mapenzi mkewake aliyemtaja kwa jina la “Mama Zakhia.”

Machozi amesema kuwa hana kinyongo na mdau huyo ingawaje kitendo hicho kilimuumiza na kumuuma mno ingawaje hakuwahi kumchana kwakuwa alikuwa anamuheshimu kupita kiasi.

“Bado namchukulia kama baba yangu na heshima yangu kwake bado haijashuka, siwezi kumchana kwasababu achiliambali kumuheshimu lakini kawaida yangu jambo likiniuma huwa naamua kukaa nalo tu moyoni,” amesema Machozi.

“Unajua, hata kama ningekuwa mimi ndo nimemfanyia yeye kitendo hicho halafu akagundua na kuniambia laivu, ingeniuma sana. Kwahiyo najichukulia ambavyo ingeniuma mimi basi najua hata kwake yeye nikimwambia pia itakuwa hivyo.”

Machozi anaamini kuwa ni shetani tu alimpitia kwa bahati mbaya mdau huyo, akisema kwamba siku zote binadamu hawakamiliki kwa kila kitu, hata yeye binafsi anaamini ana mapungufu yake hata kama hayajui.

No comments