IBRAHIM AJIB WA SIMBA AFUNGA NDOA YA UJI KWA KUMUOA MPENZI WAKE WA MUDA MREFU

MSHAMBULIAJI hatari wa Simba, Ibrahimu Ajib ameamua kuachana na ukapera kabla ya kuingia mtukufu wa Ramadhani baada ya Jumanne iliyopita kufunga ndoa, hatua ambayo ni muhimu na inamuongezea majukumu ya kimaisha.

“Cadabra” amedaiwa kuwa amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi mapema wakati waumini wa Kiislamu wakiwa wanaelekea kwenye funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Nyota huyo aliyelelewa na Simba kuanzia katika kikosi cha pili, ni mmoja wachezaji wachache hapa nchini ambao mashabiki wa soka wanamtabiria makubwa kwamba akipata nafasi ya kutoka nje ya Tanzania atakuwa na faida kubwa sana kwa soka la Tanzania.No comments