INSPECTOR HAROUN AWASHANGAA WANAOHUSISHA KIFO CHA DOGO MFAUME NA DAWA ZA KULEVYA... asema wanashindwa kujiongeza

INSPECTOR Haroun “Babu” kutoka Temeke amewashangaa watu wanaohusisha kifo cha msanii Dogo Mfaume na matumizi ya dawa za kulevya akisema kwamba wanashindwa kujiongeza.

“Kifo cha Mfaume hakijatokana na dawa za kulevya kwa sababu hadi mauti yanamkuta alikuwa tayari ameshaachana na mambo hayo kitambo na alikuwa kwenye kituo maalum kinacholea wahanga wa dawa hizo,” amesema.

“Pia ikumbukwe kuwa kifo ni mipango ya Mungu mwenyewe na vingine hivi vyote ni “visingizio” tu, kwahiyo kikubwa tunachopaswa sisi ni kumuombea mwenzetu kwani nasi hatujui kesho yetu.”

Inspector amesema kwamba kila msiba ni pengo, ila kwa upande wake anauchukulia msiba wa Dogo Mfaume kuwa zaidi ya pengo kutokana na namna tasnia ya mchiriku Bongo ilivyokuwa inamtegemea.


Mfaume amefariki dunia Jumatano, Mei 17 kutokana na tatizo la uvimbe kichwani na kuzikwa juzi Ijumaa majira ya saa saba nyumbani kwao Chanika, jijini Dar es Salaam.

No comments