JB ATETEA MAANDAMANO YA WASANII WA FILAMU YALIYOBEZWA NA NAY WA MITEGO

STAA Jacob Stephen “JB” ameonekana kupingana na baadhi ya wasanii wa bongofleva ambao wameponda tukio la kuandamana walilolifanya nyota wa filamu hivi karibuni.

JB amesema kuwa haelewi ni kwa nini watu wengine wa fani tofauti na maigizo wanabeza jitihada wanazozifanya za kuhakikisha sanaa ya Tanzania inainuka katika kipindi hiki ambapo kazi nyingi za nje zinaingia bila kufuata utaratibu.

“Sio kweli kama hatutaki kabisa kazi za nje ziingie nchini kwa kuhofia soko la filamu zetu, hapana. Sisi tunataka utaratibu ufuatwe kama ambavyo sisi wasanii wa ndani tunafanya kabla ya kuingia sokoni,” amesema JB.


JB alitoa tamko hilo baada ya rapa Nay wa Mitego kuonekana kupinga maandamano yaliyofanywa na wasanii wa filamu ili kutetea maslahi ya kazi zao. 

No comments