JOHN BOCCO ASUBIRI BARAKA ZA MANJI TU KUTUA JANGWANI MSIMU UJAO

MSHAMBULIAJI wa Azam na nahodha wa timu hiyo, John Bocco ameonyesha kila dalili ya kuondoka katika  kikosi hicho  na kinachosubiriwa sasa  ili atue Yanga ni baraka za mwenyekiti Yusuph Manji tu ili avae jezi ya ushindi msimu ujao.     

Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa mshambuliaji  huyo ni kwamba Bocco hataweza  kuichezea timu hiyo  kufuatia klabu  yake kumuonyeshea dharau  wakitaka  atemwe.

Kuthibitisha hilo juzi Bocco aliandika maneno yanayoashiria hataweza kuichezea  timu hiyo  kwa msimu ujao akisema  ni wakati wa kuchukua  maamuzi mapya ambayo ni magumu  ingawa baadae yatakuwa na manufaa.

Alipoandika  hivyo baadhi  ya wachezaji  walimuunga mkono wakimwambia  hatakuwa amekosea akifanya hivyo  akiwemo kiungo wa zamani wa Yanga, Nizar Khalfan akimtaka kutosita  kufanya hivyo kwa kuwa kuanza upya sio mbaya.

Endapo Manji  atapelekewa jina la Bocco na kukubaliana na hilo basi hakuna shaka mshambuliaji huyo atavaa jezi ya Yanga msimu ujao akipishana na Donald Ngoma ambaye bado hatma yake ya kubaki katika kikosi hicho msimu ujao haijajulikana.


Wachambuzi wa soka wanasema endapo Bocco atatua Yanga atakuwa na kazi nzuri ya kufunga mabao kutokana na soka la klabu hiyo bingwa wa mara tatu mfululizo kutumia zaidi viungo wa pembeni na mabeki wa pembeni  kulisha washambuliaji lakini pia hatua ya Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao ni kitu  kitakachomvuta kirahisi.

No comments