JONAS MKUDE ASEMA MBAO FC HAWATOKIMEI 28... adai watawachapa kama wamesimama vile

WACHEZAJI wa Simba wamesikia kwamba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeipeleka fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC ya Mwanza kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Lakini wamefurahi wakisema kwamba hata kama fainali hiyo iliyopangwa kupigwa Mei 28, mwaka huu ingepangwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba tena, wangewachapa tu waranda mbao hao.

Nahodha wa Simba, Jonas Mkude ameiambia saluti5 kwamba wamesikia fainali hiyo itapigwa kwenye uwanja huo wa makao makuu ya serikali, lakini wao wanajua kuwa wako kikazi zaidi.

“Tutawapiga kama wamesimama, watupeleke kokote pale iwe Dodoma, Mwanza, Iringa, Mbeya au Bukoba,” amesema Mkude.

Mchezaji huyo amesema kwamba hatua ya kuwapania Mbao FC sio tu inatokana na kwamba mechi dhidi yao itakuwa ya fainali bali pia ni kutokana na ukweli kwamba katika mechi ya mwisho ambayo Mbao walifungwa mabao 3-2 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Mbao walilalamika kwamba kipa wao Erick Ngwengwe alicheza chini ya kiwango.


“Sasa ili kuwaonyesha kwamba Ngwengwe wao alizidiwa na kasi ya mashambulizi, tunawasubiri kwenye fainali. Sisi sio Yanga bwana,” amesema Mkude.

No comments