JONAS MKUDE, MAVUGO WAMPAGAWISHA KIPA WA STAND UNITED

GOLIKIPA namba moja wa Stand United ya Shinyanga, Frank Mwonge amefurahishwa na kiwango walichokionesha wachezaji wawili wa Simba ambao ni Jonas Mkude pamoja na Mwinyi Kazimoto.

Akizungumza na mtandao mmoja wa michezo, kipa huyo raia wa Uganda amesema Mkede na Mwinyi walicheza vizuri sana katika nafasi zao na kuipa wakati mgumu timu yake.

“Wamejitahidi kucheza vizuri kipindi cha kwanza, Simba hawakuwa makini katika ulinzi wao lakini kukosa umakini kwa timu yetu kumechangia tufungwe."

Hata hivyo, kipa huyo amesema kwamba hakufurahishwa na jinsi mwamuzi wa mchezo huo, Imani Mwandemba kutoka Arusha alivyochezesha mchezo huo kwa sababu kulikuwa na makosa mbalimbali ambayo yaliufanya mchezo huo usiwe wa kuvutia zaidi.

“Tumekubali tumefungwa lakini mwamuzi angecheza kihalali lazima Simba tungewafunga, lakini ndiyo mchezo tunajipanga Upya.”


Timu ya Stand United inashika nafasi ya 6 ikiwa ina alama zake 36 katika msimasmo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na iliingia kwenye uwanja wa taifa kwa lengo la kushinda mechi hiyo ili kujiweka katika mazingira bora zaidi.

No comments