JOSE MOURINHO SASA AMFUNGIA KAZI KYLIAN MBAPPE


JOSE MOURINHO ameripotiwa kuwa sasa amemfanya kinda wa maajabu wa Monaco, Kylian Mbappe kuwa lengo lake kuu la usajili wa dirisha la kiangazi.
Kwa mujibu wa duru za michezo barani Ulaya Kylian Mbappe amempiku Antoine Griezmann ambaye sasa anakuwa kipaumbele namba mbili. 
Kinda huyo wa miaka 18 amekuwa akilinganishwa na nyota wa zamani wa Arsenal Thierry Henry. 
Mbappe ameifungia Monaco magoli  17 kwenye michuano yote msimu huu.

No comments