JOSEPH OMOG AJITWISHA ZIGO LA LAWAMA YA SIMBA KUKOSA UBINGWA WA LIGI KUU BARA MSIMU HUU

KOCHA wa timu ya Simba, Joseph Omog amesema kuwa yeye ndiye anayepaswa kupewa lawama baada ya kikosi chake kuipisha Yanga kubeba Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo.

Kocha huyo raia wa Camoroon amesema kuwa walifanya makosa kizembe wakati wanaongoza Ligi kiasi cha kuiachia Yanga njia nyeupe ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

“Kwa kweli tulipoteza umakini ikatugharimu lakini kama nilivyotangulia kusema hapo awali, katika hili hakuna anayestahili kulahumiwa bali mimi kama kocha ndio wa kubeba mzigo wote,” alisema kocha huyo.

“Kuna wakati inakupasa kukiri wazi baada ya kufanya makosa, tuliteleza na wenzetu wakatumia nafasi hiyo kukaa kileleni,” aliongeza Omog.


Simba ilianza vyema kwenye michuano ya Ligi Kuu bara kiasi cha kuiacha Yanga kwa jumla ya alama nane lakini mwisho wa siku mambo yamekuwa tofauti.

No comments