JUMA ABDUL ASEMA NAJERUHI YAMEMKOSESHA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MSIMU

BEKI wa timu ya Yanga, Juma Abdul amesema kuwa majeraha ya muda mrefu yamechangia kumnyima tuzo ya kuwa mchezaji bora wa msimu huu baada ya kukaa nje ya kikosi kwa muda mwingi.

Beki huyo ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Hassan Kessy, alisema kuwa unapopata majeraha unalazimika kukaa nje ya kikosi na kufanya kazi ya kupunguza mwili.

“Nilipanga kufikia mafanikio niliyoyapata msimu uliopita lakini imeshindikana kwa sababu ya jeraha nililopata na kukaa benchi muda mrefu,” alisema beki huyo.

“Hakuna mchezaji anayepanga kuwa na jeraha, ni bahati mbaya imenitokea nikashindwa kubeba tena tuzo kama nilivyofanya msimu uliopita,” aliongeza beki huyo.

“Kwa sasa nashukuru Mungu nipo kwenmye wakati mzuri baada ya kupona na kucheza vizuri kwenye mechi za mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu na kutoa mchango mkubwa kwa timu yangu.”


Juma abdul alifanikiwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliopata tuzo msimu uliopita kutoka Yanga akiwa sambamba na Thaban Kamusoko aliyebeba tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa.

No comments