JUMA LUIZIO AAMINI YANGA ITAPOROMOKA NA SIMBA ITAIBUKA NA USHINDI TU

MSHAMBULIAJI wa Simba anayecheza kwa mkopo katika kikosi hicho akitokea Zesco United ya Zambia, Juma Luizio amesema anajua kwamba Yanga wataanganguka tu na Simba watakuwa mabingwa.

Luizio ambaye amekuwa akisugua benchi katika kikosi cha Simba katika siku za hivi karibuni amesema kwamba siku zote adui yuko muombee njaa na yeye imani yake kwamba katika mechi zilizobaki Yanga lazima ataanguka.

“Yanga wanaweza kupata sare katika mechi tatu ambazo ni mbao FC, Kagera Sugar Mbeya City na pia wanaweza kufanya vibaya lakini adui yako muombee njaa tu” amesema mshambuliaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Luzio pia ametoa sababu za kukosa namba ndani ya timu hiyo kwa siku za hivi karibuni akisema sababu kubwa ni mabadiliko ya mfumo wa kocha.

“Mfumo wa mwalimu umekuwa na tatizo kwangu ndiyo maana siku hizi anamuanzisha Fredrick Blagnon kwa lengo la kutumia mpira wa juu ambapo Blagon ameonekana kuidumu vizuri kuliko mimi” emesema Luzio.

Hata hivyo amesema kwamba kila kitu kinakwenda sawa katika kikosi hicho cha Simba na Kila mchezaji amekuwa akitimizawajibu wake ipasavyo.


Simba walimsajili mchezaji huyo katika usajili wa dirisha dogo kwa mkopo wenye masharti kwamba ikimaliza msimu ulejee katika kikosi chake cha Zesco United.

No comments