JUMA NATURE AMLILIA DOGO MFAUME... asema Temeke imepoteza msanii "jembe" kwenye mchiriku

MSANII Juma Nature ameongelea kifo cha msanii mwenzie, Dogo Mfaume na kusema kuwa anasikitika kuona Wilaya ya Temeke imempoteza msanii mkali zaidi aliyekuwa vanafunika kupita wote kwenye mchiriku.

Akiongea na saluti5 Chanika, Dar es Salaam ilipofanyikia shughuli ya msiba wa Mfaume, Nature amesema kuwa Mfaume ni kati ya wasanii aliokuwa “akiwaaminia” kutokana na kuiwakilisha vyema Temeke katika muziki.

“Mfaume alikuwa msanii wa kweli na ndio maana wakati fulani aliweza hata kutwaa tuzo za muziki za Kilimanjaro, zaidi ya hilo alikuwa anajua nini anatakiwa afanye kwa wakati husika ili mashabiki wamwelewe,” amesema Nature.

Akizungumzia mwitiko mdogo wa wasanii kwenye msiba huo wa Dogo Mfaume, Nature amesema kuwa anashindwa kutoa lawama za moja kwa moja kutokana na mazingira ya umbali wa mahali yalipofanyikia maziko ukilinganisha na makali ya maisha kwa kipindi hiki.


“Hivi tunavyoongea kuna wasanii hata kupanda daladala kwao shida wanaamua tu kutembea kwa miguu, watu hawana hela nafikiri ndio sababu. Lakini hata sisi wachache tuliofika tumewawakilisha pia wala hakijaharibika kitu,” aliongeza.  

No comments