JUUKO MURSHID AHUSISHWA NA KUTAKA "KUIKIMBIA SIMBA NA KUTUA YANGA MSIMU UJAO

BEKI wa timu ya Simba, Juuko Murshid raia wa Uganda ameanza kuivuruga tena klabu yake baada ya kuanza kuhusishwa kutaka kutua Yanga msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Taarifa zilizoifikia saluti5 ni kuwa tayari ndani ya klabu ya Simba wameanza kushikana mashati baada ya beki huyo kuonekana kuanza mipango ya kuikacha timu hiyo.

Ikumbukwe beki huyo hata baada ya kumalizika kwa michuano ya AFCON nchini Gabon ambapo alikuwa na timu ya taifa ya Uganda, bado alileta usumbufu wa kurejea kikosini ilihali Simba iko kwenye kipindi kigumu wakati huu kwani beki wake tegemeo, Method Mwanjali mpaka hivi sasa hajatengemaa vizuri huku Murshid nae akionekana kuwa na akili ya kuondoka zaidi.


Klabu ya Yanga imepania kukisuka upya kikosi chake na ripoti George Lwandamina ipo mikononi mwa uongozi kwa ajili ya kufanya mageuzi msimu ujao.

No comments