Habari

KABURU ATHIBITISHA MO, POPPE HAWANA KINYONGO TENA… asema sasa ni “Nguvu Moja” kuziua Mwadui FC na Mbao

on

KAULI mbiu ya klabu ya Simba ni
maeneo mawili mazito lakini yanayoonekana ni yenye maana kubwa katika maisha ya watu wanaotamani
kupata mafanikio, “Nguvu Moja.”
Maneno haya yametumika katika vikao viwili
tofauti ndani ya siku tatu, kikao kimoja kikiwa ni cha wajumbe wa Kamati ya Utendaji
dhidi wa wajumbe wenzao, kapteni Zakaria Hans Poppe ambaye alikuwa ametangaza
kujiuzulu nafsi zake zote katika klabu hiyo.
Kamanda huyo wa zamani wa jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania alikuwa amekerwa na kitendo cha viongozi
wenzake katika Simba kuingia mkataba wenye thamani ya sh bil 4.9 na kampuni ya
Sportpesa ya Kenya.
Inadaiwa kuwa Hans Poppe
alikuwa akipinga Simba kuingia mkataba huo bila kuujadili kwa kina, lakini pia
bila kumshirikisha mwanachama mwenzao anayeisaidia Simba kwa hali na mali, “Mohammed
Dewji” “MO”.
Lakini kikao cha siku moja
baina ya viongozi na Poppe kikamaliza udhia na mwenyekiti huyo wa kamati ya
usajili akatengua uamuzi wake na kurejea kazini.
Baada ya kikao hicho wajumbe
wote wa kamati ya utendaji wakiongozwa na rais wa Simba, Evans Aveva wakafanya
kikao kingine na Mohammed Dewji ambaye naye alikuwa ametangaza mapema kwamba
hakufurahishwa na mkataba wa Sortpesa.
Taarifa ambayo imetolewa juzi na makamu wa rais wa klabu hiyo, Geofrey Nyange “Kaburu” imesema kwamba kikao
hicho na MO kilikuwa na mafanikio makubwa na wote kwa pamoja wameendelea kufuta
tofauti zao na kuongeza nguvu ya kusaidia Simba hadi mwisho.
“Tumefanya kikao na MO hakikuwa
kirefu sana lakini kilikuwa kizito. Tunashukuru kwamba ameelewa dhamira yetu
naye amekubali kwamba nia yetu ilikuwa njema kuisaidia Simba. Mambo yote
yamekwisha na tuanaendelea na jukumu letu la kuifanya Simba kuwa klabu ya
kisasa zaidi,” amesema kaburu.
Kaburu amesema kwamba kwa sasa
hakuna kiongozi yeyote katika Simba mwenye kinyongo akiwemo MO mwenyewe, na
kwamba wote wameamua kuunganisha nguvu zao kuhakikisha kwamba Simba inamaliza
mechi zake mbili zilizobaki ikiwemo ile ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC na
mwadui katika mechi ya Ligi Kuu kwa ushindi.

“Wote tumemaliza kila kitu na
kila mmoja akili yake ni kuangalia mechi zetu ile ya Jumamosi dhidi ya Mwadui
na ile ya tarehe 27 dhidi ya Mbao ambayo imeweza kutupa uwakika wa kushiriki
michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika,” amesema.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *