KABURU AWATULIZA MASHABIKI WA SIMBA AKIWAAMBIA "NDIO KWANZA KUMEKUCHA"

MAKAMU wa rais wa Simba, Geofrey Nyange “Kaburu” amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie kwani dhamira ya Simba ni kutwaaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho.

Kaburu amesema kwamba viongozi wa Simba wamefurahishwa na ushindi wa kikosi chao dhidi ya Azam FC lakini kazi bado.

Akihojiwa baada ya mchezo huo, Kaburu amesema kwamba wachezaji wa Simba wamefanya kile ambacho wanatakiwa kufanya na sasa kazi iliyobaki ni kucheza fainali.

“Wachezaji wetu wamejituma na wanastahili kupata matokeo hayo. Sasa akili yetu yote ni katika fainali dhidi ya Mbao FC,” amesema makamu huyo wa rais.


Hata hivyo mechi dhidi ya ya Azam iliharibika ladha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jana kutwaa mzima jijini Dares Salaam.

No comments