KAMUSOKO AIPA USHAURI WA BURE SIMBA SC... aitaka ipambanie kwa nguvu Kombe la FA

KIUNGO wa Yanga, Thaban Kamusoko amesema kuwa njia pekee ya klabu ya Simba kushiriki michuano ya kimataifa ni kupambana kwa nguvu zote kwenye Kombe la FA.

Kamusoko alisema kuwa anafurahia kutimiza ndoto za kubeba ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo tangu atue nchini mwaka jana.

“Hakuna namna kwa Simba, hiyo ndio hali halisi na ni bora nguvu zao sasa wazielekeze kwenye mchezo wa Kombe la FA ambao pia hauna urahisi kwasababu Mbao sio timu ya kuibeza,” alisema Kamusoko.

“Hakuna mchezaji asiyependa kubeba ubingwa mara mbili mfululizo akiwa kwenye taifa geni,” aliongeza nyota huyo.


Thaban Kamusoko alitua nchini mwaka jana na kuanza kuichezea michuano ya Ligi Kuu bara ambapo alifanikiwa kupewa tuzo ya mwanasoka bora wa kulipwa baada ya kuisaidia Yanga kubeba ubingwa wa Ligi Kuu bara na Kombe la FA.

No comments