Kundi kabambe la taarab, Ogopa Kopa Classic Band chini ya malkia wa mipasho Afrika Mashariki, Khadija Kopa litafanya onyesho kubwa mjini Bagamoyo Jumamosi ya Mei 13.

Onyesho hilo litarindima ndani ya kiota cha maraha cha Kaole Snake Park, kilichopo nje kidogo ya mji wa Bagamoyo.

Saluti5 imejulishwa kuwa hilo ni onyesho maalum la vunja jungu ambapo Ogopa Kopa watatumia fursa hiyo kutambulisha nyimbo zao mpya kabisa ukiwemo ule wa “Simpi Kiki Kunguni wa Mwendo Kasi” ulioimbwa na Mwamvita Shaibu.

Nyimbo nyingine ni “Niko Nga nga nga”  wa Young Hassan Ally, “Nadekezwa Remix” wa Prince Black Kopa  na “Nimemkinai” ulioimbwa na Naima Mohamed.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac