BEKI wa timu ya Azam FC, Shomary Kapombe amesema kuwa klabu ya Yanga ililamba dume kuinasa saini ya Hassan Kessy ambaye alikuwa akiitumikia Simba msimu uliopita.

Kapombe amesema kuwa Kessy anaimarika kadri siku zinavyozidi kwenda na ndie mtu pekee anayeweza kurithi nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa.

“Niweke wazi tu kuwa msimu huu sikuwa vizuri sana kwasababu ya hali ya majeruhi ya muda mrefu, lakini kama ni kura yangu naipeleka kwa Kessy wa Yanga.”

“Ni mchezaji ambaye yuko vizuri, anaweza kukamata nafasi yangu kwenye timu ya taifa, anaimarika kadri siku zinavyozidi kwenda,” aliongeza.

Shomary Kapombe ndie beki tegemeo kwenye kikosi cha Azam na timu ya taifa lakini kwa muda mrefu alikuwa nje ya kikosi kutokana na matatizo ya kiafya.

Hassan Kessy alisajiliwa kutoka Simba ambapo usajili wake ulileta zogo kubwa nchini, huku wekundu wa Msimbazi wakishikilia msimamo kwamba bado walikuwa na mkataba nae kabla ya kuidhinishwa Yanga.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac