KIBA AJIBU MAPIGO YA UJASIRIAMALI YA DIAMOND PLATNUMZ... nae kujikita kwenye biashara ya mavazi na vinywaji

BAADA ya staa wa bongofleva, Daiamond Platnumz kuzindua perfume yake, msanii mwenzake ambaye ana upinzani nae mkubwa, Ali Kiba amekuja na mkakati wa kuanzisha biashara ya mavazi aina ya jeans, miwani, viatu na vinywaji vyenye jina lake.

Kiba amesema kuwa mipango hiyo ni mizito na hatarajii kuifanya kiholela kwani hata mwanzo alifanya kama promosheni lakini sasa hivi hayuko tayari kukosea hatua yoyote.

“Nina mipango mikubwa nje ya muziki, nataka kuanzisha biashara kubwa ya mavazi, miwani, viatu na vinywaji vyenye jina langu,” alisema Kiba.

“Viatu, miwani na jeans vitatoka hivi karibuni kwasababu kila kitu kimekamilika, kisha baadae nitaleta vinywaji vyenye kuongeza nguvu vyenye jina langu,” ameongeza msanii huyo.


Kumekuwa na ushindani mkubwa kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba kiasi cha kuwagawa mashabiki wa bongofleva kwenye makundi mawili makubwa.

No comments