KIKOSI CHA SIMBA CHAJICHIMBIA JESHINI KUIVUTIA KASI AFRICAN LYON

KIKOSI cha Simba kiko mawindoni kikiwa kimeweka kambi kwenye viwanja vya chuo cha polisi jijini Dar es Salaam.

Wekundu hao wameweka kambi kwenye viwanja vya jeshi hilo la polisi kwa ajili ya mechi yao ya Jumapili dhidi ya African Lyon pia ya jijini Dar es Salaam.

“Baada ya Jumamosi iliyopita Simba kutinga fainali ya Kombe la FA, Jumanne kikosi cha timu hiyo kiliingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya African Lyon utakaochezwa Jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam,” imesema taarifa rasmi.

Taarifa hiyo ikasema kwamba Simba imeingia kambini katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ya Ndege Beach iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi la Simba, amesema kikosi chao kitakuwa kikifanya mazoezi hapo mara mbili kwa siku ambapo asubuhi kitakuwa katika uwanja ulioko ndani ya kambi hiyo na jioni kitakuwa kwenye uwanja wa chuo cha polisi kilichopo Kurasini.

“Tumeamua kuweka kambi katika viwanja hivi vya jeshi kutokana na utulivu mkubwa ulioko humu,” amesema kiongozi huyo.


Katika mechi za Ligi Kuu, Simba inalazimika kupigania kushinda mechi zake tatu zilizobaki dhidi ya Lyon, Mwadui FC na Stand United, lakini pia huku ikipiga magoti kuomba sana Yanga wateleze katika mechi zao zilizobaki.

No comments