KINGWENDU: WASANIII TUNAKUFA VIFO VYA GHAFLA, CHANGAMKIENI FURSA YA KUPIGA PICHA NA WASANII KABLA HAWAJAFARIKI


MCHEKESHAJI Rashid Mzange “Kingwendu” amewataka mashabiki kuwa na utamaduni wa kupenda kupiga picha na wasanii ili kuweza kubaki na kumbukumbu hasa pale inapotokea wasanii hao kupoteza maisha.

Akiongea na saluti5, Kingwendu amesema kuwa, ni vyema mashabiki wakawa na utaratibu huo kwa mara kwa mara, kutokana na kile alichokidai kuwa wasanii wengi wamekuwa wakifa vifo vya ghafla.

“Unapopata fursa ya kupiga picha na msanii, iwe wa filamu, muziki ama wa fani yoyote ile, basi unatakiwa kuichangamkia kutokana na kuwa sisi wasanii tumekuwa tukifa vifo vya ghafla vinavyofanya tuwaache mashabiki wetu bila kumbukumbu,” amesema Kingwendu.

Mchekeshaji huyo amesema kwamba yuko tayari kusimamishwa hata njiani na shabiki wake ambaye atataka kupiga nae picha ya ukumbusho na kwamba anayemwitaji kwa hilo asisite kumwambia.

No comments