KIPA NAMBA TATU WA YANGA ASEMA HAONI TATIZO KUKALIA BENCHI... asema siku hazigandi "one day yes"

KIPA wa timu ya Yanga, Beno Kakolanya amesema kuwa haoni tatizo kwake kuwekwa benchi na George Lwandamina kwasababu yeye ndie mwenye dhamana ya kupanga kikosi cha kwanza katika kila mchezo.

Kakolanya alijiunga na Yanga msimu huu akitokea Tanzania Prisons ya Mbeya ambapo amekuwa akipigania namba mbele ya deogratius Munishi “Dida” na Ally Mustafa “Barthez” ambao hutumika mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza.

“Tangu mwanzo watu walikuwa wanasema siwezi kupata namba Yanga lakini wanasahau kuwa mpaka hivi sasa nimeshacheza mechi nne kwenye kikosi cha kwanza na nimefanya vizuri,” alisema kipa huyo.

“Kucheza mechi nne kikosi cha kwanza mbele ya wazoefu wawili sio jambo dogo, hasa kwa nafasi zetu za makipa ambazo hazifanyiwi mabadiliko ya mara kwa mara,” aliongeza.

“Kocha yuko sahihi na naamini kadri siku zinavyokwenda nitapewa mechi zaidi na kupata uzoefu mkubwa, nafanya mazoezi, siamini kama naweza kushuka kiwango.”


Klabu ya Yanga iliamua kumsajili kipa huyo ili kuongeza hali ya ushindani kwenye nafasi ya mlinda mlango ambayo kwa muda mrefu ilitawaliwa na makipa wawili am,bao ni Dida na Barthez.

No comments