KIPA SERGIO ROMERO AONYESHA VITU ADIMU MAN UNITED IKITOA SARE KWA SOUTHAPTON

Sergio Romero amekuwa nyota wa mchezo kwenye mechi ya Premier League iliyoshuhudia Southampton ikiikaribisha Manchester United na kuibana kwa sare ya 0-0.
Kipa huyo wa kimataifa wa Argentina aliokoa mashuti mengi ikiwemo penalti ya dakika ya tano. Ilikuwa ni kama mechi iliyotoa kipimo halisi kuwa anastahili kucheza fainali ya Europa League Mei 24.
Aliruka kushoto na kulia kupangua mikwaju iliyoonekana dhahiri kuelekea wavuni.
SOUTHAMPTON: Forster, Soares (Pied 69), Stephens, Yoshida, Targett,Ward-Prowse (Boufal 77), Romeu, Davis, Redmond, Gabbiadini (Rodriguez 62), Tadic
MANCHESTER UNITED: Romero, Bailly, Smalling, Jones, Darmian, Mkhitaryan, Tuanzebe (Carrick 64), Fellaini (Herrera 75), Mata (Rashford 69), Rooney, Martial

No comments