KIPRE TCHETCHE APATA KIGUGUMIZA KUWEKA WAZI KAMA ATARUDI KUKIPIGA BONGO

ALIYEKUWA mchezaji wa Azam FC, Kipre Tcheche ameshindwa kufuta uvumi unaomhusisha kurejea nchini na kujiunga na timu ya Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Tcheche aliondoka nchini na kutimkia Falme za Kiarabu ambapo mpaka hivi sasa hakuna mchezaji mbadala ambaye ameweza kuziba nafasi yake vyema.

“Siwezi kukana au kuthibitisha taarifa hizo kwasababu kwenye mpira lolote linaweza kutokea, hivyo hata mimi kujiunga na Yanga halitakuwa jambo la kushangaza,” alisema mshambuliaji huyo.

“Napokea simu nyingi toka kwenye timu za Tanzania lakini ni mapema mno kuthibitisha habari hizo kwasababu sifahamu kesho mambo yatakuwaje,” aliongeza.


Tcheche kuondoka kwake Azam kuligubikwa na sintomfahamu kwani hakuwa amemaliza mkataba wake na mabingwa hao wa Kombe la mapinduzi hali iliyopelekea kuwepo kwa mtafaruku.

No comments