KITALE KUBADILISHA STAILI YA UIGIZAJI WAKE... sasa kucheza kama "mpemba"

MSANII anaecheza kama "Teja" au "Mkude Simba", Mussa Kitale amesema ameamua kubadili aina ya uigizaji wake na muda si mrefu kuanzia sasa ataonekana akiigiza kama ‘Mpemba’.

Akielezea sababu zilizomfanya abadili aina ya uigizaji huo, Kitale amesema, anawafahamu vilivyo Wapemba kwa sababu tabia zao hazijatofautiana na Waruguru ambao ndio asili yake.

“Nitaweza tu kuwaigiza kwa sababu Waruguru na Wapemba wanafanana tabia wabish. Hata kama jambo sio la ukweli watakufosi uamini la kweli”, alisema Kitale.  


Kitale amewahakikishia mashabiki wake kuwa wasubiri kazi nzuri kutoka kwake kwani huwa hakosei.

No comments