KITALE NAE AFICHUA SIRI YA KUMUDU KWAKE KUIGIZA KAMA “TEJA”


MSANII wa maigizo ambae pia ni mwimbaji, Mussa Kitale amefichua siri inayomfanya aweze kumudu kuvaa vilivyo uhusika wa ‘teja’ katika uigizaji wake.

Akiongea na saluti5, Kitale alisema kuwa maisha yake yote toka utotoni  amekulia uswahilini, Tandale na nyumbani kwao kulikuwa na kambi ya wahuni “mateja” hivyo alikuwa akiona maisha yao wanavyoishi.

“Sijawahi kutumia kilevi cha aina yoyote na sio muhuni, mimi ni mfuasi mzuri wa dini ya kiislamu pia ni mwalimu wa madrasa,” alisema Kitale.


Alisema, ameamua kuigiza kama teja ili kubeba uhalisia, kufikisha ujumbe pamoja na kutoa elimu kuhusiana na ulevi huo hatari unaoharibu maisha ya vijana wengi nchini kwa sasa.

No comments