KIUNGO WA MBAO FC AMMIMINIA SIFA HARUNA NIYONZIMA... asema ameshindwa kugundua udhaifu wake

PAMOJA na ushindi walioupata Mbao FC katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Yanga, kiungo wa timu hiyo Salmin Hoza amesema kuwa hakuna mtu anayeweza kujifananisha na Mnyarwanda Haruna Niyonzima kwa wachezaji wanaocheza nafasi ya katikati ya uwanja.

Kiungo huyo amesema kuwa Tanzania pana wachezaji wengi na bora ila Niyonzima ndio mchezaji pekee aliyejaa ubunifu mkubwa uwanjani.

“Kama kuna mchezaji msumbufu unapokutana nae katikati basi ni Haruna Niyonzima wa Yanga, jamaa msumbufu na anacheza kwa akili sana,” alisema nyota huyo. 

“Sio kwamba Tanzania Hakuna mchezaji mwenye uwezo hapana lazima tukubali jamaa ni mbunifu sana ni vigumu kumkabili unapokumbana naye” aliongeza.

“Nimecheza kwa muda mrefu na nimekumbana na viungo wengi lakini Niyonzima ni habari nyingine, nimeshindwa kujua ubunifu wake”.

Nyota huyo amekumbana na Yanga kwenye michezo miwili mmoja waLigi Kuu Bara na mwingine wa Kombe la FA ambapo alisema kuwa Niyonzima ndiye mchezaji pekee nchini ambaye ameshindwa kugundua udhaifu wake.


Mbao wamefanikiwa kuingia hatua ya fainali ambapo watakumbana na Simba katika mchezo uliopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

No comments