KIVURANDE ASEMA KIBAO KATA KIMEMPA FAIDA ASIYOITARAJIA IKIWEMO KUPANDA NDEGE... ajivunia kufanya kazi na Sabah Muchacho, Khadija Kopa, Diamond Platnumz

MFALME wa Kibao Kata, Jumaa Kivurande amefichua kwamba kujiunga kwake na aina hiyo ya muziki kumempa faida nyingi na kemkemu, ikiwa ni pamoja na kumuweka karibu na mashabiki na baadhi ya mastaa wakubwa wa muziki Bongo.

Akiongea katika kipindi cha Mitikisiko ya Pwani ndani ya Times FM chini ya Khadija Shaibu “Dida”, Kivurande amesema kuwa katika maisha yake hakuwahi kufikiri kama iko siku atafanya kazi na wasanii kama Sabah Muchacho, Khadija Kopa na Diamond Platnumz.

“Nimepanda ndege mimi Dida kwa ajili ya Kibao Kata, nimesafiri hadi Dubai kwa ajili ya Kibao Kata kwa hiyo nashukuru sana,” amesema Kivurande ambaye hivi karibuni anatarajiwa kuachia kibao cha mduara kiitwacho “Moyo Kama Macho”.

Msanii huyo amesema kuwa, anachokifanya hivi sasa ni kuzidisha heshima na nidhamu kwa mashabiki na wadau, hasa awapo jukwaani, ili kuwavuta karibu zaidi na kuwafanya waendelee kumsapoti.

No comments