KIVURANDE WA KIBAO KATA ASEMA AMEOA MAPEMA ILI KUKWEPA VISHAWISHI VYA MABINTI

MFALME wa Kibao Kata, Kivurande Junior amefunguka na kusema kuwa ameoa mapema ili kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kumfanya atumbukie kwenye maradhi kutokana na watoto wa kike wengi kumfuata kwa kasi wakimtaka kimapenzi.

Msanii huyo alivuta jiko ndani mwishoni mwa mwaka jana huku akidai kuwa ameharakisha mno kufanya hivyo lakini sababu kubwa ikiwa ni kuwakata maini mabinti waliokuwa wakimuingiza kwenye majaribu.

“Tangu nipate umaarufu nimekuwa nikijikuta naingia kwenye vishawishi ambapo wanawake wamekuwa wakinighasi kila uchao hadi wakati mwingine nilikuwa nikilazimika kuzima simu yangu kuwakwepa,” amesema.

“Lakini sasa hivi tayari nina jibu la kumpa yeyote yule atakayejaribu kuniingiza kwenye kishawishi kwa kumuweka wazi kuwa sina mpango huo kwa kuwa mimi ni mume wa mtu.”

No comments