KIVURANDE WA KIBAO KATA AWAPA "TANO" MASHABIKI WANAOMSAPOTI

MFALME wa Kibao Kata, Kivurande Junior anaetamba hivi sasa na wimbo wa "Moyo Kama Macho" ameshukuru mashabiki kwa kuupokea vyema wimbo wake huo aliouachia wiki mbili zilizopita.

Akiongea na saluti5, Kivurande amesema amepata mafanikio mengi kupitia kibao hicho ikiwemo mialiko ya kutumbuiza sehemu mbalimbali ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam.

“Baada ya wimbo huu nitaachia ngoma nyingine  itakayokwenda kwa jina la "Nimekupa Moyo Wangu" ambao nao naamini utafunika kama ulivyo huu wa "Moyo Kama Macho",” amesema Kivurande.


Kivurande ni kati ya wasanii wa muziki walioko juu zaidi kwa sasa hapa Bongo, kutokana na kukubalika kwake kwa kasi kwa mashabiki na wapenzi mbalimbali.

No comments