KOCHA JOSEPH OMOG WA SIMBA ACHEMKA KUINASA SAINI YA KIUNGO KENNY ALLY WA MBEYA CITY

MIPANGO ya kocha  wa Simba, Joseph Omog kuinasa saini ya kiungo wa Mbeya City, Kenny Ally imegonga mwamba baada ya meneja wa mchezaji huyo, Maka Mwalwisi kusisitiza kuwa haondoki mwishoni mwa msimu huu.

Omog alikuwa kwenye mipango ya kumnasa Kenny ili kuziba nafssi ya Jonas Mkude ambaye anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu ambapo amepanga kutimkia Afrika Kusini kucheza soka la kulipwa.

“Mbeya City ni pahala salama zaidi kwake kuliko kumpeleka sehemu ambayo anaweza kuhatarisha uwezo wake kwa kuwekwa benchi,”alisema meneja huyo.

“Hii ni sehemu ambayo anapata mechi za kutosha na kumjenga kuliko kwenda sehemu ambayo anaweza kujikuta anaanzia benchi,”aliongeza.


Kamati ya usajili ya kikosi hicho ilikuwa kwenye mawindo ya siri ili kuinasa saini yake na hii ni baada ya wekundu hao kushindwa na Jonas Mkude aliyetaka mzigo mkubwa wa hela awekewa mezani.

No comments