KOCHA LWANDAMINA AKABIDHI MAJINA SABA YA WACHEZAJI WA NDANI YA YANGA ANAOWAHITAJI TENA MSIMU UJAO

LIGI Kuu Tanzania Bara na Kombe la FA vikiwa vinaelekea ukingoni kumalizika, kocha wa timu ya Yanga, George Lwandamina ametoa orodha ya majina saba ya wachezaji wa ndani kwa Kamati ya mashindano kwa ajili ya kufanya nao kazi msimu ujao.

Yanga ambayo baadhi ya wachezaji muhimu wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu wakiwemo Haruna Niyomzima, Vicent Bosou, Nadir Haroub Canavaro, Donald Ngoma na Thaban Kamusoko, inaonekana kuanza mapema kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.

Wapo baadhi ya wachezaji ambao watatemwa mwishoni mwa msimu huu kulingana na ripoti ya Lwandamina lakini yapo majina ya wachezaji muhimu ambayo kocha anataka kuendelea nao akiwa tayari amekabidhi kwa Kamati ya mashindano.

“Ni mapema mno kuweka wazi wachezaji ambao nitaendelea nao msimu ujao kwani suala hilo tayari nimeliwasilisha kwenye Kamati ya mashindano kwa ajili ya utekelezaji,” alisema kocha huyo.

"Kila mmoja anajua kuwa nilichukua timu katikati ya msimu, nataka kufanya mabadiliko makubwa msimu ujao ndio maana nimeanza kuandaa mazingira mapema,” aliongeza kocha huyo raia wa Zambia.

No comments