KOCHA LWANDAMINA AWAPA WACHEZAJI WA YANGA WOSIA WA "UBINGWA" MSIMU HUU

KOCHA Geogre Lwandamina raia wa Zambia amekitazama kikosi chake na kutoa wosia ambao kama utazingatiwa na wachezaji, Yanga inaweza kuibuka na ubingwa mwishoni mwa msimu huu baada ya kuchanga vyema karata zake.

Lwandamina amesema amewataka wachezaji wa kikosi hicho kusahau yote yaliyotokea kwenye klabu hiyo na kuweka akili zao kwenye kubeba ubingwa wa Ligi Kuu bara ambao bado upo wazi. “Nimewataka wachezaji watulize akili zao wapambane uwanjani kwasababu ya heshima ya klabu” alisema kocha huyo.

“Yanga ni sehemu salama zaidi kwao wanapaswa kuweka akili zao uwanjani tu bila kujali nini kilitokea, hiyo itakuwa njia salama ya kubeba ubingwa na kurejea kwenye michuano ya kimataifa,” aliongeza.

Timu hiyo ambayo Jumamosi ilikuwa uwanjani kucheza na Prison ya Mbeya imebakiza mechi zake dhidi ya timu za Toto African, Mbeya City Mbao FC na Kagera Sugar.


Katika mechi zote hizo Yanga itakuwa ugenini moja tu dhidi ya Mbao FC huku michezo mingine wakicheza kwenye uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam.

No comments