KOCHA LWANDAMINA AZUIA NIYONZIMA KUONDOKA YANGA... asema bado yuko kwenye mipango yake

KIUNGO wa kimataifa wa timu ya Yanga, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda ambaye mkataba wake unatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi ujao, bado yuko kwenye mipango ya kocha wa timu hiyo, George Lwandamina.

Habari kutoka ndani ya yanga zinasema kuwa nyota huyo anahitajika na kocha Lwandamina hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kupewa mkataba mpya.

“Ni kweli mkataba wake unaisha mwezi ujao, lakini ni vigumu sana kwake kuondoka kwasababu bado yuko kwenye mipango ya mwalimu,” kilisema chanzo cha taarifa hii.

“Jina lake lipo kwenye orodha ya wachezaji ambao kocha anataka kuendelea nao msimu ujao na kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.”


Haruna ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda, amechezea Yanga kwa mafanikio makubwa na amekuwa chachu ya mataji kwa timu hiyo baada ya kuibebesha makombe ya Ligi Kuu Bara zaidi ya mara tatu mfululizo. 

No comments