KOCHA PLUIJIM ACHARUKA SINGIDA UNITED... apanga kuwanasa nyota wengine watatu wa kimataifa

KOCHA wa timu ya Singida United, Hans Pluijim amepania kukitia makali kikosi chake baada ya kuingia kwa nguvu kwenye soko la usajili huku akipanga kuwanasa nyota wengine watatu wa kimataifa.

Pluijim hivi karibuni alikamilisha usajili wa beki wa Uganda, Shafik Batambuze na kumpa mkataba wa miaka miwili akitokea kwenye klabu ya Tusker FC ya Kenya.

“Tunataka kuingia Ligi Kuu kwa staili ya tofauti, hatutaki kwenda kushiriki ila tunataka kwenda kupambana, hivyo ni lazima tufanye maandalizi ya kutosha,” alisema mratibu wa klabu hiyo, Sanga Festo.

“Bado hatujakamilisha idadi ya wachezaji wa kigeni kama TFF inavyotaka, tunahitaji kuongeza nyota wengine watatu wenye uzoefu,” aliongeza.

Timu ya Singida United imeshakamilisha usajili wa wachezaji watatu kutoka Zimbabwe ambao ni Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa na Twafaza Kutinyu.


Timu hiyo ni miongoni mwa zile tatu zilizopanda daraja msimu huu kwa ajili ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao, nyingine zikiwa ni Njombe Mji na Lipuli FC ya Iringa. 

No comments